Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Wanazuoni Waislamu wa Lebanon katika kikao chake cha kawaida imesema: Adui Mzayuni anaendelea na uvamizi wake na umefikia hatua ya kutaka kuwaua viongozi wa Hamas waliokuwa wakisimamia mazungumzo, ilhali walikuwa wakijadili mpango wa Trump uliowasilishwa kwao katika nchi yenye uhusiano wa nusu wa kawaida na adui Mzayuni, huku ukipuuzia misingi yote ya kidiplomasia na kisheria inayopaswa kulinda wajumbe waliishiriki mazungumzo.
Jumuiya hyo imesisitiza kuwa shambulizi hili liliendeshwa kwa uratibu kamili na Marekani, jambo lililo wazi katika taarifa ya adui Mzayuni aliyesema kwamba aliwajulisha Marekani kuhusu operesheni hii na akapokea idhini, hata hivyo, Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa adui, alidai kwamba alitekeleza jambo hili peke yake bila uratibu na Marekani na kwamba yeye binafsi ndiye anabeba jukumu lote, huenda hili lilikuwa kutokana na kushindwa kwa operesheni ya kuwaua viongozi wa Hamas, hata hivyo, jambo hili halipaswi kupita bila kuwajibishwa.
Jumuiya ya wanazuoni ilisema: Serikali ya Qatar inapaswa kwanza kuchukua hatua rasmi za kukata uhusiano na utawala wa Kizayuni.
Jumuiya hyo mesisitiza kuwa operesheni hii inathibitisha kwamba Benjamin Netanyahu hataki vita vya Ghaza vimalizike, haangaiki na Wazayuni waliotekwa nyara, na anaona kubaki kwake madarakani ni muhimu zaidi kuliko kila kitu kingine, hata kama itahatarisha mustakabali wa nchi yake na Wazayuni.
Jumuiya a Wanazuoni wa Lebanon imeongeza kusema: jambo hili limethibitishwa na gazeti la Kiyahudi la Haaretz lililoandika kuwa; Netanyahu alibashiri juu ya shambulizi la Qatar kwamba litamuokoa katika siku zijazo, lakini hatua hiyo iliongeza hatari kwa waliotekwa.
Jumuiya hiyo wa wanazuoni imesisitiza: Tunamshukuru Mungu kwamba muqawama upo tayari uwanjani na kwa operesheni shujaa karibu na mji wa Ramot iliyosababisha kuuawa Wazayuni saba na kujeruhiwa wengine saba, na pia kupitia ndege zisizo na rubani kutoka Yemen zilizolenga viwanja vya ndege vya utawala wa Kizayuni na kupelekea hasara za binadamu na mali katika uwanja wa ndege wa Ramot, walimuonesha adui Mzayuni ladha ya kushindwa.
Maoni yako